HISPANIA imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa Olympia Jijini Berlin nchini Ujerumani.
Nyota mwenye asili ya Ghana, Nicholas ‘Nico’ Williams Arthuer (22) alianza kuwafungia La Roja dakika ya 47 akimalizia pası nzuri ya winga mwenzake mwenye asili ya Afrika, Lamine Yamal Nasraoui Ebana (17) ambaye baba yake anatokea Morocco na mama yake, Sheila Ebana anatokea Equatorial Guinea.
Lakini Cole Jermaine Palmer (22) akaisawazishia Three Lions dakika ya 72 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake mshambuliaji, Jude Victor William Bellingham baada ya kazi nzuri ya Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka mwenye asili Nigeria, Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka.
Shujaa wa Hspania alikuwa ni winga pia, Mikel Oyarzabal Ugarte aliyefunga bao la ushindi dakika ya 86 baada ya kazi nziri ya beki wa Chelsea, Marc Cucurella Saseta.
Hilo linakuwa taji la nne kwa Hispania baada ya awali kulitwaa katika miaka ya 1964, 2008 na 2012, wakati kwa England hii ni mara ya pili wanafungwa katika Fainali kufuatia 2020 walipokuwa wenyeji kuchapwa kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Italia Uwanja wa Wembley Jijini London.
0 comments:
Post a Comment