// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JKU YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 MWENGE KOMBE LA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JKU YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 MWENGE KOMBE LA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 12, 2024

    JKU YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 MWENGE KOMBE LA KAGAME


    TIMU ya JKU ya Zanzibar imefufua matumaini ya kufanya vyema kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa JKU, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya KMC yamefungwa na Nassoro Matta dakika ya 28 na Veva Adeline dakika ya 86 na kwa ushindi huo mabingwa hao wa Zanzibar wanaokota pointi tatu za kwanza kufuatia kufungwa 1-0 na Hay Al Wadi ya Sudan katika mchezo wa kwanza.
    Coastal Union inabaki na pointi zake tatu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Dekedaha ya Somalia kwenye mchezo wa kwanza hapo hapo Uwanja wa KMC. 
    Jioni hii, Hay Al Wadi inaumana na Dekedaha, wakati baadaye Saa 12:00 jioni SC Villa itamenyana na Singida Black Stars na Saa 3:00 usiku APR itamenyana na El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini, zote zikiwa mechi za Kundi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKU YAIKANDA COASTAL UNION 2-0 MWENGE KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top