KIUNGO Farid Mussa Malik leo amemkabidhi jezi namba 17 mchezaji mpya, Mzambia Clatous Chota Chama aliyesajiliwa kutoka kwa watani, Simba SC.
Farid amekuwa akivaa jezi namba 17 tangu akiwa Azam FC alipodumu kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 alipokwenda Tenerife B alikocheza hadi mwaka 2020 alipojiunga na Yanga na kuendelea kutumia jezi hiyo.
Kwa upande wake Chama amekuwa akitumia jezi namba 17 tangu anawasili Simba SC mwaka 2018 kutoka Lusaka Dynamos ya kwao, Zambia hadi alipouzwa RS Berkane mwaka 2021 alikocheza hadi 2022 akaendelea kuvaa jezi hiyo hadi anaachana na klabu hiyo mwezi uliopita.
0 comments:
Post a Comment