WACHEZAJI wanane, wakiwemo beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' na viungo Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' wa Azam FC na Stephane Aziz Ki wa Yanga, raia wa Burkina Faso wameingia kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2023-2024.
Wengine ni makipa Djigui Diarra wa Yanga, raia wa Mali na Leyi Matampi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mabeki Ibrahim Abdallah Hamad 'Bacca' na Kouassi Attohoula Yao na winga, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon wa Azam, wote raia wa Ivory Coast.
Tuzo za wachezaji na timu zilizofanya vizuri katika Ligi Kuu msimu uliopita zitafanyika Agosti 1 kwenye ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment