// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, July 16, 2024

    AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ


    KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mshambuliaji, Cheickna Diakite (19) kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali.
    Huyo anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine ni beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien.
    Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia.
    Kuna wazawa pia wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma.
    Aidha, Azam FC pia imemnunua moja kwa moja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa wa Kimataifa was Sudan, Mohamed Mustafa kutoka El Merreikh ya Sudan.
    Hatua hiyo inafuatia kazi nzuri ya kipa huyo kufuatia kusajiliwa kwa mkopo mwezi Januari akiisaidia Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top