// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC KUZINDUA JEZI MPYA KWENYE BOTI YA KILIMANJARO VIII KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC KUZINDUA JEZI MPYA KWENYE BOTI YA KILIMANJARO VIII KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 31, 2024

    AZAM FC KUZINDUA JEZI MPYA KWENYE BOTI YA KILIMANJARO VIII KESHO


    KLABU ya Azam kesho inatarajiwa kutambulisha jezi zake za msimu mpya kwa staili ya aina yake – Saa 3:00 Asubuhi watafanya uzinduzi kwenye boti ya Kilimanjaro VIII ‘The Falcon Sea’ Jijini Dar es Salaam, kabla ya Saa 9 Alasiri kufanya utazinduzi jengo la Michenzani Mall, Unguja.
    Katika hatua nyingine, kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kurejea usiku wa mapema asubuhi ya kesho kutoka Morocco kilipokuwa kimeweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya.
    Azam FC wanatarajiwa kuuanza msimu mpya kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union ya Tanga Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Ikiwa Morocco, Azam FC pia ilicheza mechi tatu za kujipima nguvu, Julai 20 ikishinda 3-0 dhidi ya Union Yacoub El Mansour, Julai 27 ikitoa sare ya 1-1 na Union de Touarga, kabla ya kuchapwa 4-1 na Wydad Athletic FC Julai 29. 
    Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika – itakuwa na safari ya Rwanda pia kucheza na wenyeji, Rayon Sports katika mchezo mwingine wa kirafiki. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC KUZINDUA JEZI MPYA KWENYE BOTI YA KILIMANJARO VIII KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top