// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC KUCHEZA NA WYDAD MECHI YA KIRAFIKI JULAI 29 MOROCCO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC KUCHEZA NA WYDAD MECHI YA KIRAFIKI JULAI 29 MOROCCO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 19, 2024

    AZAM FC KUCHEZA NA WYDAD MECHI YA KIRAFIKI JULAI 29 MOROCCO


    KLABU ya Azam FC inatarajiwa kuanza kucheza mechi za kirafiki katika kambi yake ya nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya, ambao wataufungua kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya jamii dhidi ya Coastal Union visiwani Zanzibar.
    Mechi ya kwanza watacheza Jumamosi dhidi ya timu ya Daraja la Tatu, Union Yacoub El Mansour, kabla ya Julai 27 kumenyana na Union de Touarga na kumaliza kwa kumenyana na mabingwa wa kihistoria wa Morocco, Wydad Athletic Julai 29.
    Azam FC imeweka kambi Morocco kujiandaa na msimu mpya baada ya kufanya usajili mkubwa kuboresha kikosi chake.
    Imesajili wachezaji saba wapya ambao ni beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na viungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien, kiungo mshambuliaji, Cheickna Diakite (19) kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali.
    Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia.
    Kuna wazawa pia wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma.
    Aidha, Azam FC pia imemnunua moja kwa moja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa wa Kimataifa was Sudan, Mohamed Mustafa kutoka El Merreikh ya Sudan.
    Hatua hiyo inafuatia kazi nzuri ya kipa huyo kufuatia kusajiliwa kwa mkopo mwezi Januari akiisaidia Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA NA WYDAD MECHI YA KIRAFIKI JULAI 29 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top