KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo Awesu Ally Awesu (27) kuwa mchezaji wake mpya wa 14 kuelekea msimu ujao, akijiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kutoka KMC, zote za Dar es Salaam.
Wachezaji wengine 13 walioswajiliwa Simba ni mabeki, Kelvin Sospeter Kijiri (24) kutoka Singida Big Stars, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya (DRC), wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
Kikosi cha Simba SC kwa sasa kipo mjini Ismailia nchini Misri ambako kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment