// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); APR YAENDELEZA UBABE KOMBE LA KAGAME, YAICHAPA EL MERREIKH 1-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE APR YAENDELEZA UBABE KOMBE LA KAGAME, YAICHAPA EL MERREIKH 1-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, July 13, 2024

    APR YAENDELEZA UBABE KOMBE LA KAGAME, YAICHAPA EL MERREIKH 1-0


    BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Mauritania, Mamadou Sy dakika ya 70 jana lilitosha kuipa APR ya Rwanda ushindi wa 1-0 dhidi ya El Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi C Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    APR inafikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Singida Black Stars katika mchezo wa kwanza, wakati El Merreikh Bentiu inabaki na pointi yake moja kufuatia sare ya bila mabao na SC Villa yenye pointi nne sasa nafasi ya pili katika mchezo wa kwanza.
    Singida Big stars ambayo jana ilipoteza mechi ya pili mfululizo baada ya kuchapwa 3-1 na SC Villa ndiyo inashika mkia Kundi C. 
    Jana jioni ilichezwa mechi moja ya Kundi A na JKU ya Zanzibar ilifufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa JKU, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya JKU yalifungwa na Nassoro Matta dakika ya 28 na Veva Adeline dakika ya 86 na kwa ushindi huo mabingwa hao wa Zanzibar wanaokota pointi tatu za kwanza kufuatia kufungwa 1-0 na Hay Al Wadi ya Sudan katika mchezo wa kwanza.
    Coastal Union inabaki na pointi zake tatu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Dekedaha ya Somalia kwenye mchezo wa kwanza hapo hapo Uwanja wa KMC. 
    Washindi wa kwanza wa kila Kundi A, B na C ndiye watafuzu Nusu Fainali wakiungana na mmoja kati ya washindi wa pili Bora wa makundi yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: APR YAENDELEZA UBABE KOMBE LA KAGAME, YAICHAPA EL MERREIKH 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top