MABAO ya Mohamed Abdelrahman Yousif dakika ya 22 na 27 yaliipa Al Hilal Omdurman ya Sudan ushindi wa 2-0 dhidi ya ASAS ya Djibouti katika mchezo wa Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, bao la mkongwe James Chamanga dakika ya 74 lilitosha kuipa Red Arrows ya Zambia ushindi wa 1-0 dhidi ya Gor Mahia hapo hapo Azam Complex.
0 comments:
Post a Comment