TIMU ya Taifa ya Ureno imeanza vyema Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2020’ baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo wa Kundi F usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig nchini Ujerumani.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa Ureno kwani ililazimika kutoka nyuma baada ya winga wa Slavia Prague, Lukáš Provod kuanza kuifungia Jamhuri ya Czech dakika ya 62 na ndipo beki wa Viktoria Plzeň, Robin Hranáč akajifunga dakika ya 69 kuipatia ‘A Seleção das Quinas’ bao la kusawazisha, kabla ya winga wa Porto, Francisco Fernandes da Conceição kuifungia timu yake bak la ushindi dakika ya 90’+2.
Mechi iliyotangulia ya Kundi F Uturuki waliichapa Georgia 3-1 Uwanja wa Westfalenstadion Jijini Dortmund.
Mabao ya Uturuki yalifungwa na beki wa Fenerbahçe, Mert Müldür dakika ya 25, winga wa Real Madrid, Arda Güler dakika ya 65 na kiungo mshambuliaji wa Galatasaray, Muhammed Kerem Aktürkoğlu dakika ya 90’+7, wakati bao pekee la Georgia lilifungwa na mshambuliaji wa Metz ya Ufaransa, Georges Mikautadze dakika ya 32.
0 comments:
Post a Comment