• HABARI MPYA

    Sunday, June 30, 2024

    UJERUMANI NA USWISI ZATINGA ROBO FAINALI EURO 2024, ITALIA 'OUT'


    TIMU za Uswisi na wenyeji, Ujerumani jana wamefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baada ya kuzitoa Italia na Denmark.
    Mabao ya kiungo wa Bologna, Remo Freuler dakika ya 37 na winga wa FC Augsburg, Rubén Vargas dakika ya 46 Uwanja wa Olympia Berlin Jijini Berlin yaliipa Uswisi wa ushindi wa 2-0 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Italia.
    Nao Ujerumani pia wakaitupa nje Denmark kwa kuichapa 2-0, mabao ya viungo washambuliaji, Kai Havertz wa Arsenal dakika ya 53 kwa penalti na Jamal Musiala wa Bayern Munich dakika ya 68 Uwanja wa BVB Jijini Dortmund.
    Hatua ya 16 Bora Euro 2024 inaendelea leo kwa michezo mingine miwili, England na Slovakia Saa 1:00 usiku na Hispania na Georgia Saa 4:00 usiku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJERUMANI NA USWISI ZATINGA ROBO FAINALI EURO 2024, ITALIA 'OUT' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top