• HABARI MPYA

    Sunday, June 23, 2024

    UBELGIJI YAZINDUKA, URENO YAENDELEZA UBABE EURO 2024 RONALDO 'WA MOTO'


    UBELGIJI imezinduka jana baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Romania katika mchezo wa Kundi E Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 usiku wa jana Uwanja wa Cologne Jijini Cologne nchini Ujerumani.
    Mabao ya Ubelgiji jana yalifungwa na viungo wanaocheza Ligi Kuu ya England, Youri Marion Tielemans wa  Aston Villa dakika ya pili na Kevin De Bruyne dakika ya 79.
    Kwa matokeo hayo sasa timu zote za Kundi E zina pointi tatu na mechi za mwisho ndizo zitaamua timu za kwenda Hatua ya 16 Bora, Ubelgiji wakimaliza na Ukraine na Slovakia dhidi ya Romania Jumatano Saa 1:00 usiku.
    Mechi nyingine za jana za Kundi F; Ureno iliichapa Uturuki 3-0, mabao ya Bernardo Silva dakika ya 21, Samet Akaydin aliyejifunga dakika ya 28 na Bruno Fernandes dakika ya 55 akimalizia pasi ya Cristiano Ronaldo aliyeendelea kung'ara jana 
    na Georgia ikatoa sare ya 1-1 na Czechia Uwanja wa Volkspark Jijini Hamburg.
    Matokeo hayo yanamaanisha Ureno iliyofikisha pointi sita imetinga Hatua ya 16 Bora, wakati Uturuki yenye pointi tatu, Czechia na Georgia zenye pointi moja kila moja baada ya wote kucheza mechi mbili zitasubiri hatima zao kwenye mechiza mwisho Jumatano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UBELGIJI YAZINDUKA, URENO YAENDELEZA UBABE EURO 2024 RONALDO 'WA MOTO' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top