TIMU ya Simba Queens imekabidhiwa Kombe lao ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2023-2024 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Queens Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Asha Juma Mnunka dakika ya tatu hilo likiwa bao lake la 20 la msimu, Elizabeth Mwambui dakika ya 35 na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika ya 79.
Simba Queens ilijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake wikiendi iliyopita baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Fountain Gate Princess hapo hapo Azam Complex ilipofikisha pointi 49 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine na leo imeongeza tatu na kuwa 52.
0 comments:
Post a Comment