TIMU za Kenya, Zambia na Nigeria ndizo nchi tatu za Afrika zitakazoiwakilisha Afrika kwenye michuano ya nane ya Kombe la Dunia la FIFA kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 inayotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 16 hadi Novemba 3 mwaka huu Jamhuri ya Dominica.
Nigeria itakwenda kwenye Fainali hizo kwa mara ya sita ikiwa timu pendwa zaidi Afrika, huku Zambia ikipewa heshima pia kwa kiwango chao kizuri katika michuano iliyopita, wakati kwa Kenya wanakwenda kushiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Flamingos ya Nigeria ilikata tiketi yake baada ya kuitoa Liberia kwa jumla ya mabao 6-1, wakishinda 4-1 ugenini na 2-0 nyumbani, Abuja, wakati Zambia Copper Princesses wa Zambia imefuzu kwa kuitoa Morocco kwa jumla ya 3-1, ushindi walioupata nyumbani baada ya sare ya bila mabao Morocco na Kenya, Harambee Starlets waliitoa Burundi jijini Nairobi kwa jumla ya mabao 5-0.
Fainali za Kombe la Dunia la FIFA U17 2024 zitashirikisha timu tatu za Afrika pamoja na England, Brazil, Colombia, Ecuador, Hispania, Marekani, Japan, Mexico, New Zealand, Poland, Jamhuri ya Watu wa Korea, Jamhuri ya Korea na wenyeji Jamhuri ya Dominica.
0 comments:
Post a Comment