• HABARI MPYA

    Tuesday, June 25, 2024

    MZAMIRU YASSIN AONGEZA MKATABA MPYA SIMBA SC HADI MWAKA 2026


    KIUNGO Mzamiru Yassin Selemba (28) amesaini mkataba wa mpya wa miaka miwili kuendelea na kazi Simba SC hadi mwaka 2026.
    Rasmi, Mzamiru anakuwa mchezaji wa kwanza kutajwa kuongeza mkataba Simba SC baada ya wengine sita kuachwa na kusajili mpya mmoja.
    Walioachwa ni mabeki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.
    Aidha, tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MZAMIRU YASSIN AONGEZA MKATABA MPYA SIMBA SC HADI MWAKA 2026 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top