RASMI JKT Tanzania imenusurika kushuka Daraja baada ya sare ya bila mabao na Tabora United katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
JKT imenufaika na ushindi mnono wa ugenini, mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na sasa Tabora United watakwenda kumenyana na Biashara United ya Mara kutoka Championship kwa michezo mingine miwili ya nyumbani na ugenini kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment