KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Mamelodi Sundowns Ijumaa.
Wachezaji waliosafiri ni makipa; Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata, mabeki; Nahodha Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Yao Attohoula Kouasi, Nickson Kibabage, Joyce Lomalisa, Gift Fred na Kibwana Shomari.
Viungo ni; Khalid Aucho, Zawadi Mauya, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli, Pacome Peodoh Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Augustine Okrah, Mahlatse Skudu Makudubela, Farid Mussa na Denis Nkane, wakati washambuliaji ni Clement Mzize, Joseph Guede na Kennedy Musonda.
Yanga SC watakuwa wageni wa Mamelodi Sundowns Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria.
Yanga inahitaji ushindi au sare ya mabao ili kwenda Nusu Fainali kufuatia sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment