TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutwaa Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Fainali usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Msenegal, Babacar Sarr, dakika ya 77 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Israel Patrick Mwenda kufuatia mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana kuangushwa nje kidogo ya boksi.
Kwa ushindi huo, Simba SC imezawadiwa Sh. Milioni 50, wakati washindi wa pili, Azam FC wamepata Sh. Milioni 30.
Hilo linakuwa taji la pili kwa Simba SC msimu huu baada ya kuanza na taji la Ngao ya Jamii wakimfunga mtani, Yanga Agosti mwaka jana Jijini Tanga.
Hilo linakuwa taji la pili kwa Simba SC msimu huu baada ya kuanza na taji la Ngao ya Jamii wakimfunga mtani, Yanga Agosti mwaka jana Jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment