MSHAMBULIAJI Mkongo wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele leo ametembelea kambi ya Simba SC Jijini Cairo ikijiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly kesho Uwanja wa Cairo international.
Simba watakuwa wageni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho kuanzia Saa 5:00 usiku Uwanja wa Cairo international wakikabiliwa na shinikizo la kushinda ugenini kufuatia kufungwa 1-0 na mabingwa hao watetezi kwenye mechi ya kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla katí ya Al Ahly na Simba atakwenda kumenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.
Mayele alijiunga na Pyramids Julai 30, mwaka jana akitokea Yanga SC ya Tanzania pia ambako alisajiliwa Agosti 1, mwaka 2021 kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa.
0 comments:
Post a Comment