MABINGWA watetezi, Manchester City usiku wa jana wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji ‘bwana mdogo’ wa miaka 23, Muingereza Philip Walter Foden aliyefunga mabao matatu dakika za 45, 62 na 69 kufuatia kiungo Mspaniola, Rodrigo Hernández Cascante ‘Rodri’ kufunga la kwanza dakika ya 11, wakati bao pekee la Aston Villa lilifungwa na Jhon Jader Durán Palacio.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 30, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao tu na Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Na wote wapo nyuma ya Arsenal ambao wanaongoza kwa pointi 68 baada ya kucheza mechi 30.
0 comments:
Post a Comment