TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao ya Mtibwa Sugar, timu kutoka kijiji cha Lusanga, Manungu, Turiani mkoani Morogoro yamefungwa na Abdul Hillary dakika ya 70 kwa penalti na Omary Marungu dakika ya 76.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 18, ingawa inaendelea kushika mkia na Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 sasa nafasi ya nane.
0 comments:
Post a Comment