KLABU ya Yanga imesema hakutakuwa na kiingilio kwa mashabiki wa eneo la Mzunguko kwenye mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Jumamosi ya Machi 30 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba uongozi umeamua eneo la mzunguko watu waingie bure.
Aidha, Kamwe ametaja viingilio vya maeneo mengine kuwa ni Sh. 𝟏𝟎,𝟎𝟎𝟎
Kwa 𝐕𝐈𝐏 C, Sh. 𝟐𝟎,𝟎𝟎𝟎 𝐕𝐈𝐏 B na 𝟑𝟎,𝟎𝟎𝟎 kwa 𝐕𝐈𝐏 A.
“Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la mzunguko litakuwa bure,” amesema Kamwe.
Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment