WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 28, Feisal Salum, mawili dakika ya 63 na 64 na winga mzawa, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 69.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidwa wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi tatu mkononi.
Kwa upande wao Dodoma Jiji baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 18 nafasi ya 12.
0 comments:
Post a Comment