MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Polisi Tanzania katika Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Kwa upande wao, washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC watamenyana na Green Warriors, wakati vigogo Simba SC walioishia Nusu Fainali watakutana na TRA ya Kilimanjaro na mechi zitachezwa kati ya Februari 19 na 20.
Yanga wakifanikiwa kuitoa Polisi Tanzania watakutana na mshindi kati ya Biashara United na Dodoma Jiji, wakati Azam FC wakiitoa Green Warriors watakutana na mshindi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United na Simba wakiitoa TRA watakutana na mshindi kati ya Mashujaa na Mkwajuni FC katika Hatua ya 16 Bora.
0 comments:
Post a Comment