TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyewe, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 16 kwa penalti kufuatia mshambuliaji Kibu Dennis kuanguka kwenye boksi.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 11, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 31 za mechi 13 na Yanga pointi 31 za mechi 12.
Kwa upande wao Mashujaa hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupoteza mechi hiyo, wakibaki na pointi zao tisa za mechi 13 sasa nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, mkiani wakiwa Mtibwa Sugar wenye pointi nane za mechi 14.
0 comments:
Post a Comment