MABINGWA watetezi, Manchester City usiku wa jana wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mshambuliaji Muingereza mzaliwa wa Kingston, Jamaica, Raheem Sterling alianza kuifungia Chelsea dhidi ya timu yake ya zamani dakika ya 42, kabla ya kiungo wa Kimataifa wa Hispania, Rodrigo ‘Rodri’ Hernández kuisawazishia Manchester City dakika ya 83.
Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 53 katika mchezo wa 24, ingawa wanabaki nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal yenye pointi 55 na Liverpool 57 baada ya wote kucheza mechi 25.
Kwa upande wao Chelsea baada ya sare hiyo wanabaki na pointi zao 35 za mechi 25 nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment