TIMU ya Liverpool jana ilirejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley FC Uwanja Anfield Jijini Liverpool.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 31, Luis Díaz dakika ya 52 na Darwin Núñez dakika ya 79, wakati bao pekee la Burnley lilifungwa na Dara O'Shea dakika ya 45.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 24 na kuendelea kuongoza ligi hiyo mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 52bza mechi 23, wakati Arsenal sasa ni ya tatu ikiwa na pointi zake 49 za mechi 23.
kwa upande wao Burnley baada ya kichapo cha jana wanabaki na pointi zao 13 za mechi 24 nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20.
0 comments:
Post a Comment