WENYEJI, Arsenal jana wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Washika Bunduki yalifungwa na Sven Botman aliyejifunga dakika ya 18, Kai Havertz dakika ya 24, Bukayo Saka dakika ya 65, Jakub Kiwior dakika ya 69, wakati bao pekee la Newcastle United lilifungwa na Joe Willock dakika ya 84.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 58, ingawa wanabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 59 na Liverpool wenye pointi 60, wakati Newcastle United inabaki na pointi 37 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 26.
0 comments:
Post a Comment