WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro ametembelea Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San Pedro, Ivory Coast ili kuona ambavyo nchi hiyo imefanya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu.
Waziri Dk. Ndumbaro amefanya hivyo ili kujifunza namna ambavyo Ivory Coast wamefanikiwa naye ajifunze kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za mwaka 2027 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.
Dk. Ndumbaro amesema aina ya uwanja aliouona unafaa pia katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo amesema Serikali mbali na kuendelea kujenga viwanja vya michezo Dodoma na Arusha inaendelea kukaribisha wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo katika ujenzi wa miundombinu ya michezo katika mikoa mingine.
Katika ziara hiyo, Dk. Ndumbaro aliambatana na Kaimu Balozi wa Kituo cha Abuja anayehudumia pia nchi ya Ivory Coast, Judika Nagunwa, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay na Maafisa wengine wa Wizara.
0 comments:
Post a Comment