// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS NA ZAMBIA ZATOLEWA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS NA ZAMBIA ZATOLEWA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 25, 2024

    TAIFA STARS NA ZAMBIA ZATOLEWA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA


    TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa bastará imetupwa nje Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika licha ya sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa mwisho wa Kundi F usiku wa jana Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo nchini Ivory Coast.
    Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F, Morocco iliichapa Zambia 1-0, bao pekee la kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Hakim Ziyech dakika ya 37 Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro.
    Morocco inamaliza na pointi saba kileleni ikifuatiwa na DRC yenye pointi tatu na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora, wakati Zambia iliyomaliza na pointi tatu nafasi ya tatu sasa na Tanzania zinaaga mashindano hayo.
    Mechi za mwisho za Kundi E jana zote zilimalizika kwa sare ya bila mabao,Afrika Kusini na Tunisia Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly na Namibia dhidi ya Mali Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro.
    Mali imeongoza Kundi E kwa pointi zake tano, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye pointi nne na zote zimefuzu Hatua ya 16 Bora, huku Namibia iliyoshika nafasi ya tatu na kuzidiwa wastani wa mabao tu na Bafana Bafana ikiungana na Tunisia iliyoshika mkia na pointi zake mbili kurejea nyumbani.
    Hatua ya 16 Bora itaanza Jumamosi; Angola na Namibia Saa 2:00 usiku usiku na Nigeria na Cameroon Saa 5:00 usiku, Jumapili Equatorial Guinea na Guinea Saa 2:00 usiku na Misri na DRC Saa 5:00 usiku.
    Jumatatu itakuwa ni katí ya Cape Verde na Mauritania Saa 2:00 usiku na Senegal dhidi ya Ivory Coast Saa 5:00 usiku, wakati Jumanne ni Mali na Burkina Faso Saa 2:00 usiku na Morocco dhidi ya Afrika Kusini Saa 5:00 usiku. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS NA ZAMBIA ZATOLEWA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top