KIKOSI cha Yanga SC leo kimenya mazoezi ya mwisho kuuzoea Uwanja wa Baba Yara Jijini Kumasi nchini Ghana tayari kwa mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Medeama kesho Saa 1:00 usiku.
Katika mechi zake mbili za mwanzo, Yanga ilifungwa 3-0 CR Belouizdad na Novemba 24 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers na sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly Desemba 2 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao, Medeama mechi ya kwanza walichapwa 3-0 pia na Al Ahly Novemba 25 Jijini Cairo, kabla ya kushinda 2-1 nyumbani dhidi ya CR Belouizdad Desemba 1.
0 comments:
Post a Comment