KLABU ya Yanga imetupwa nje ya kinyang'anyiro cha Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika, huku kocha mpya wa wapinzani, wao Simba SC, Mulgeria Abdelhak Benchika akiingia Fainali ya Tuzo Kocha Bora wa Mwaka.
Katika Tuzo hizo zitakazotolewa Jumatatu ya Desemba 11, jina la Yanga litatajwa kupitia mshambuliaji wake wa zamani, Mkongo Fiston Kalala Mayele aliyeingia Fainali ya kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
Mayele ambaye kwa sasa anachezea Pyramids ya Misri ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuiwezesha Yanga kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake saba.
Benchika ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuiwezesha USM Alger kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kwa kuizidi Yanga kete Yanga kwa kanuni ya mabao ya ugenini, kufuatia sare ya jumla ya 2-2, akishinda 2-1 Dar es Salaam na kufungwa 1-0 Algiers.
Sherehe za utoaji wa Tuzo hizo zitafanyika ukumbi wa Palais des Congrès, uliopo ndani ya hoteli Movenpick, Jijini Marrakech nchini Morocco usiku wa Jumatatu kuanzia Saa 1:00 usiku.
ORODHA YA WANAOWANIA TUZO:
MCHEZAJI BORA WA KIUME
Mohamed Salah (Egypt, Liverpool)
Achraf Hakimi (Morocco, Paris Saint-Germain)
Victor Osimhen (Nigeria, Napoli)
MCHEZAJI BORA WA KIKE
Asisat Oshoala (Nigeria, Barcelona)
Thembi Kgatlana (South Africa, Racing Louisville)
Barbara Banda (Zambia, Shanghai Shengli)
MCHEZAJI BORA WA KIUME ANAYECHEZA AFRIKA:
Fiston Mayele (DR Congo, Pyramids)
Peter Shalulile (Namibia, Mamelodi Sundowns)
Percy Tau (South Africa, Al Ahly)
MCHEZAJI BORA WA KIKE ANAYECHEZA AFRIKA:
Refilwe Tholakele (Botswana, Mamelodi Sundowns)
Fatima Tagnaout (Morocco, AS FAR)
Lebohang Ramalepe (South Africa, Mamelodi Sundowns)
KOCHA BORA WA KIUME
Abdelhak Benchika (Algeria, Simba SC)
Walid Regragui (Morocco)
Aliou Cisse (Senegal)
KOCHA BORA WA TIMU ZA WANAWAKE:
Reynald Pedros (Morocco)
Desiree Ellis (South Africa)
Jerry Tshabalala (South Africa, Mamelodi Sundowns)
KIPA BORA WA KIUME
Andre Onana (Cameroon, Manchester United)
Mohamed El Shenawy (Egypt, Al Ahly)
Yassine Bounou (Morocco, Al Hilal)
KIPA BORA WA KIKE
Khadija Er-Rmichi (Morocco, AS FAR)
Chiamaka Nnadozie (Nigeria, Paris FC)
Andile Dlamini (South Africa, Mamelodi Sundowns)
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA KIUME
Abdessamad Ezzalzouli (Morocco, Real Betis)
Lamine Camara (Senegal, Metz)
Amara Diouf (Senegal, Metz)
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA KIKE
Comfort Yeboah (Ghana, Ampem Darkoa)
Nesryne El Chad (Morocco, Lille)
Deborah Abiodun (Nigeria, Pittsburgh Panthers)
TIMU BORA YA TAIFA WANAUME
Gambia
Morocco
Senegal
TIMU BORA YA TAIFA WANAWAKE
Morocco
Nigeria
South Africa
KLABU BORA WANAUME
Al Ahly (Egypt)
Wydad Athletic Club (Morocco)
Mamelodi Sundowns (South Africa)
KLABU BORA WANAWAKE
AS FAR (Morocco)
Sporting Casablanca (Morocco)
Mamelodi Sundowns (South Africa)
0 comments:
Post a Comment