MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (wanaume) Afrika kufuatia kuisaidia Napoli kutwaa taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33 - akifunga mabao 26 katika mechi 32 alizocheza na timu hiyo ya Italia, huku pia akifunga bao lililoiwezesha Napoli kutwaa ubingwa wa ligi mwezi Mei.
Osimhen amewashinda Mohamed Salah wa Misri na Achraf Hakimi wa Morocco katika tuzo hiyo na kuwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kushinda tuzo hiyo tangu Nwankwo Kanu ashinde mwaka 1999.
Mnigeria mwingine, Asisat Oshoala, alishinda Mwanasoka Bora wa kike baada ya kufanya vizuri akiwa na Barcelona ya Hispania na timu yake ya taifa.
ORODHA KAMILI YA WASHINDI
Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanaume): Victor Osimhen (Nigeria, Napoli)
Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanawake): Asisat Oshoala (Nigeria, Barcelona)
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu (Wanaume): Percy Tau (Afrika Kusini, Al Ahly)
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu (Wanawake): Fatima Tagnaout (Morocco, AS FAR)
Kocha Bora wa Mwaka (Wanaume): Walid Regragui (Morocco)
Kocha Bora wa Mwaka (Wanawake): Desiree Ellis (Afrika Kusini)
Kipa Bora wa Mwaka (Wanaume): Yassine Bounou (Morocco, Al Hilal)
Kipa Bora wa Mwaka (Wanawake): Chiamaka Nnadozie (Nigeria, Paris FC)
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka (Wanaume): Lamine Camara (Senegal, Metz)
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka (Wanawake): Nesryne El Chad (Morocco, Lille)
Timu ya Taifa ya Mwaka (Wanaume): Morocco
Timu ya Taifa ya Mwaka (Wanawake): Nigeria
Klabu Bora ya Mwaka (Wanaume): Al Ahly (Misri)
Klabu Bora ya Mwaka (Wanawake): Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
0 comments:
Post a Comment