TIMU ya Liverpool imekamilisha mechi zake za Kundi E katika UEFA Europa League kwa kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji, Royale Union Saint-Gilloise usiku wa jana Uwanja wa Lotto Park Jijini Brusells, Ubelgiji.
Mabao ya yalifungwa na mshambuliaji Mualgeria Mohammed Amoura dakika ya 32 na kiungo Mspaniola mzaliwa wa Uswisi,
Cameron Puertas dakika ya 43, wakati la Liverpool limefungwa na beki chipukizi Muingereza, Jarell Quansah dakika ya 39.
Pamoja na kichapo hicho bado wanamaliza vinara wa Kundi hilo kwa pointi zao 12, wakifuatiwa na Toulouse ya Ufaransa pointi 11 na wote wanasonga mbele.
Kwa upande wao Royale Union Saint-Gilloise waliomaliza na pointi nane nafasi ya tatu na LASK ya Austria iliyomaliza mkiani na pointi zake tatu zote zimeaga michuano.
0 comments:
Post a Comment