TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa Awesu Awesu dakika ya pili, Waziri Junior dakika ya 10 na Daruwesh Saliboko dakika ya 71, wakati ya Mashujaa yamefungwa na Abdulnasir Issa dakika ya 15 na Adam Adam dakika ya 20.
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya nne, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nane za mechi tisa nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment