SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifutia klabu ya Simba adhabu ya kutofanya usajili hadi baada ya kuilipa klabu ya Teungueth ya Senegal sehemu ya mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho kwenda QRM ya Ufaransa.
FIFA iliifungia Simba kufanya usajili hadi itakapoilipa klabu ya Teungueth sehemu ya mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho iliyemuuza US Quevilly-Rouen, ama US Quevilly, au QRM ya Ufaransa.
Winga huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Simba SC Agosti mwaka 2021 akitokea Teungueth FC ya kwao, Senegal na baada ya misimu miwili mizuri akaondoka Msimbazi kwenda QRM inayoshiriki Ligi ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa, Ligue 2.
0 comments:
Post a Comment