KLABU ya Yanga imeingia kwenye orodha ya mwisho ya timu tano kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika katika dola ya Wanaume ikichuana na USM Alger ya Algeria, Al Ahly ya Misri, Wydad Athletic ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Aidha, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele aliyesaidia Yanga kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ameingia kwenye 10 Bora ya kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
Yanga ilitoa sare ya jumla ya 2-2 na USM Alger waliotwaa ubingwa kwa Sheria ya mabao ya ugenini kufutia kushinda 2-1 Dar es Salaam na kufungwa 1-0 Algiers.
Kipa wa Kimataifa wa Mali na Yanga aliyeingia kwenye vipengele viwili vya awali, Kipa Bora na Mchezaji Bora Anayecheza Afrika hakuvuka hatua ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment