RAIS wa Yanga, Hersi Ally Said ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Klabu za Soka Afrika katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Marriot Mena House, Cairo.
Chama cha Klabu za Afrika kinalenga kuwaleta pamoja wadau kutoka nyanja mbalimbali za soka barani Afrika, kukuza ushirikiano, uvumbuzi na ubora ndani ya eneo la soka la klabu za bara hili, hili likiwa wazo la Rais wa CAF mwenyewe, Dk Motsepe alipokutana na Wenyekiti wa klabu za Afrika Oktoba5, 2023 na kuwaarifu kuhusu kuundwa kwa Chama hichokwa malengo yafuatayo:
1. kulinda na kukuza maslahi ya Vilabu vya Soka vya Afrika.
2. kuhakikisha kuwa Vilabu vya Soka vya Afrika vina uwezo wa kibiashara, ushindani wa kimataifa na kuleta faida
3. kuhakikisha kuwa Waamuzi, Kamishna wa Mechi na waendeshaji VAR wanaheshimiwa, wanaaminika, wanajitegemea na wa kiwango cha kimataifa.
4. kujenga ubia na wafadhili, sekta binafsi na Serikali kujenga viwanja vinavyoendana na viwango vya CAF na FIFA na miundombinu na vifaa vingine vya mpira wa miguu katika kila moja ya Vyama 54 Wanachama wa CAF.
5. kuendeleza vipaji vya vijana wa Kiafrika, akademi za Wavulana na Wasichana na kuboresha ubora wa soka la Klabu za Kiafrika kuwa za kiwango cha kimataifa.
0 comments:
Post a Comment