WENYEJI, Tottenham Hotspur jana wamechapwa mabao 4-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
Ilikuwa ni siku nzuri kwa mshambuliaji Msenegal, Nicolas Jackson mzaliwa wa Gambia aliyefunga mabao matatu dakika za 75, 90+4 na 90+7 baada ya kiungo Cole Palmer kufunga la kwanza, ambalo lilikuwa la kusawazisha kufuatia Dejan Kulusevski kuanza kuifungia Spurs dakika ya sita.
Ikawa siku zaidi kwa Spurs iliyoanza mapema kufuatia mabeki wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, Cristian Romero dakika ya 33 Destiny Udogie dakika ya 55.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ifikishe pointi 15 na kusogea nafasi ya 10, wakati Tottenham Hotspur inayobaki na pointi zake 26 inashukia nafasi ya pili baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa msimu ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 11.
0 comments:
Post a Comment