TIMU ya Arsenal imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya kuchapwa mabao 3-1 na West Ham United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora usiku wa Jumatano Uwanja wa London.
Mabao yaliyoipeleka West Han United Robo Fainali yamefungwa na Ben White aliyejifunga dakika ya 16, Mohammed Kudus dakika ya 50 na Jarrod Bowen dakika ya 60, wakati la kufuatia machozi la Arsenal limefungwa na Martin Odegaard 90.
0 comments:
Post a Comment