MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, RB Leipzig katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Red Bull Arena mjini Leipzig.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden dakika ya 25, Julian Alvarez dakika ya 84 na Jeremy Doku dakika ya 90 na ushei, wakati la RB Leipzig limefungwa na Lois Openda dakika ya 48.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi G kwa pointi tatu zaidi ya RB Leipzig wote wakiwa mbele ya Young Boys na Red Star Belgrade zenye pointi moja kila moja.
0 comments:
Post a Comment