WENYEJI, Brighton & Hove Albion wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The Amex, Falmer, East Sussex.
Mabao ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Simon Adingra dakika ya 20 na beki Muingereza, Lewis Carl Dunk dakika ya 78, wakati ya Liverpool yote yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 40 akimalizia pasi ya Darwin Núñez na dakika ya 45 na ushei.
Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Brighton & Hove Albion inafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi nane.
0 comments:
Post a Comment