BAADA ya kufanyiwa vipimo vya kina, ni rasmi sasa nyota wawili wa Azam FC, kiungo mzawa Yahya Zayd na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube watakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu kila mmoja.
Wachezaji hao walilazimika kufanyiwa mabadiliko ya haraka kipindi cha kwanza, Azam FC ikiichapa Singida Fountain Gate mabao 2-1, kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Dube anasumbuliwa na majeraha ya nyonga, huku Zayd akiwa amechanika kiraba (meniscus) kinachokuwa katikati ya goti, kinacholiimarisha lisikwaruzane.
Kiraba hicho pia huwezesha goti kufanya kazi vizuri kwa maana ya kukunja na kukunjua.
Wachezaji hao wanaendelea na programu ya kutibu majeraha yao chini ya uangalizi wa Mtaalamu wa tiba za viungo (physiotherapist) wa timu yetu, Joao Rodrigues.
0 comments:
Post a Comment