WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ametembelea Kambi ya mazoezi ya Klabu ya Yanga, Avic Town jijini Dar es Salaam ambayo inajiandaa na mchezo wa marudiano wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Timu ya Al-Merreikh ya nchini Sudan utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam. Septemba 30, 2023.
Waziri Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza timu hiyo kwa matokeo mazuri ya mchezo wa kwanza nchini Rwanda akiwataka waendeleze ushindi huo kesho ili waendelee kuitangaza vyema Klabu hiyo na Tanzania na kupata nafasi ya kusonga mbele zaidi kuingia hatua ya makundi.
"Nawapongeza wachezaji Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Abdulla Baka ambao ni Mabeki wa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Algeria ambao umeipa nafasi Tanzania kufuzu AFCON mwaka 2024 nchini Ivory Coast " Amesisitiza Mhe. Ndumbaro.
Kwa upande wake Rais wa timu hiyo, Mhandisi Hersi Said ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na nchi za Kenya na Uganda kuhakikisha nchi hizo zinashinda kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027).
Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia ameipongeza timu hiyo akiitaka iendeleze ushindi wa awali na akibainisha kuwa katika Mashindano ya mwakani Tanzania itaingiza timu nne.
0 comments:
Post a Comment