KIUNGO wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi (20) amejiunga na klabu ya FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji.
Baada ya kuibukia katika akademi ya Azam FC, Miroshi alichezea Biashara United katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kabla ya kwenda Israel mwaka 2021 ambako alichezea timu za vijana za Maccabi Tel Aviv na Beitar Tel Aviv Bat Yam hadi mwaka jana alipouzwa Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment