WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Dominik Szoboszlai dakika ya tatu, Matthew Cash aliyejifunga dakika ya 22 na Mohamed Salah dakika ya 55.
Kwa ushindi huo, Wekundu hao wanafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Aston Villa wanabaki na pointi zao sita nafasi 11 baada ya wote kucheza mechi nne.
0 comments:
Post a Comment