• HABARI MPYA

        Thursday, September 14, 2023

        CHANGALAWE AMTWANGA MUALGERIA NA KUTINGA FAINALI KUFUZU OLIMPIKI PARIS 2024


        BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania amefanikiwa kutinga Fainali ya Mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki mwakani Paris baada ya ushindi wa Refa Kusimamisha Pambano (RSC) kumuokoa mpinzani, Mualgeria Younes Nemouchi katika pambano la uzito wa Light Heavy leo Jijini Dakar nchini Senegal.
        Nemouchi mwenye umri wa miaka 29 na aliyewahi kufuzu na kushiriki mashindano yaliyopita ya Olimpiki ya Tokyo 2020 aliokolewa na refa katika Raundi ya tatu baada ya kusukumiwa makonde mfululizo bila majibu na Changalawe.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: CHANGALAWE AMTWANGA MUALGERIA NA KUTINGA FAINALI KUFUZU OLIMPIKI PARIS 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry