BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania amefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki ya mwakani Jijini Paris kwa Afrika baada ya kumshinda Mpi Anauel Ngamissengue wa Kongo Brazzaville kwa points 5-0 uzito wa Light Heavy leo Jijini Dakar nchini Senegal.
Kwa ushindi huo, Changalawe ameingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya kufuzu Paris Olimpiki 2024 yanayoendelea katika Jiji la Dakar, Senegal ambapo jumla ya nafasi za awali 18 za kufuzu kushiriki Olimpiki kwa Bara la Afrika zinagombewa.
Awali ya hapo, Zulfa Macho Yussuf alipoteza pambano lake la 16 Bora leo mchana mbele ya Adeiola Oyesiji wa Nigeria kwa points 5-0.
Sasa Tanzania imebakiwa na mabondia wanne ambao bado wanaendelea kusaka nafasi za kufuzu - wengine Changalawe, Abdallah Katoto na Grace Mwakamele.
Baada ya Dakar, yatafuatia mashindano mawili ya kidunia ya kufuzu yatakayofanyika mwakani ambapo jumla ya nafasi 100 zitagombaniwa katika michezo itakayofanyika Busto Arsizio, Italy na Bangkok, Thailand.
0 comments:
Post a Comment