• HABARI MPYA

        Monday, September 11, 2023

        BONDIA MWINGINE WA TANZANIA ATINGA ROBO FAINALI KUFUZU OLIMPIKI


        BONDIA machachari wa Tanzania, Abdallah Abdallah ‘Katoto’ amefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Mashindano ya kufuzu Olimpiki baada ya ushindi dhidi ya Abdallah Saied Nasser Emam wa Misri kwa pointi 5-0 uzito wa Fly leo Jijini Dakar, Senegal.
        Huyo anakuwa bondia wa tatu wa Tanzania kuingia Robo Fainali ya kuwania nafasi ya kwenda Olimpiki ya Paris mwakani - wengine ni Yussuf Changalawe na Grace Mwakamele.
        Bondia mwingine wa Tanzania aliyecheza leo awali Musa Maregesi alipoteza kwa pointi dhidi ya mwenyeji, Kebe Karamba uzito wa Cruiser.
        Kesho ni siku ya mapumziko katika michezo hii ya kuwania nafasi za kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 inayoendelea Dakar, Senegal. 
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: BONDIA MWINGINE WA TANZANIA ATINGA ROBO FAINALI KUFUZU OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry